FREE FLAVA

Like us on Facebook..!

FIND G5 ON

ADVERTISEMENT

Top 3 Photos Today

2. women seeking for men in mumbai

Added by Koku Tibaimuka on October 21, 2013

3. IMG_20150819_233418

Added by Benni Ashuza Vs Bab-G Ally on September 17, 2015

Top 5 Videos this Week

Nyaraka za Bin Laden zafichua mvutano baina ya al-Qaeda na washirika wake

Nyaraka zilizopatikana kutoka nyumbani kwa Osama bin Laden huko Abbottabad, Pakistan, zinaonesha kuwa jumuiya yake ilikuwa na matatizo ya kuyadhibiti matawi yake ulimwenguni kote, hasa vitendo vilivyopelekea mauaji ya Waislamu.

Mvulana wa Kisomali akiangalia mabaki ya gari iliyokuwa na bomu lililolipuka kwenye barabara yenye harakati nyingi karibu na makazi ya raisi mjini Mogadishu hapo tarehe 21 Machi. Maafisa waliwalaumu al-Shabaab kwa shambulizi hilo. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]

Mvulana wa Kisomali akiangalia mabaki ya gari iliyokuwa na bomu lililolipuka kwenye barabara yenye harakati nyingi karibu na makazi ya raisi mjini Mogadishu hapo tarehe 21 Machi. Maafisa waliwalaumu al-Shabaab kwa shambulizi hilo.Nyaraka hizo, ambazo zilitolewa hadhari siku ya Alhamis (tarehe 3 Machi), zinaonesha kuwa kiongozi huyo wa zamani wa al-Qaida alikuwa anaelewa athari hasi kwa hadhi ya al-Qaida kutokana na mashambulizi ya watu wake wa karibu na washirika wake.

Kushuka kwa hadhi ya al-Qaeda kutoka kwa umma kulimpelekea hata kufikiria kubadilisha jina la jumuiya yake.
Somalia

Nyaraka hizo zinaonesha kuwa mauaji na upigaji mabomu uliokuwa unafanywa na al-Shabaab kulikuwa chanzo cha kumfanya bin Laden awe na wasiwasi, ambapo alikataa ombi la kikundi hicho kutangaza hadharani kuwa ni washirika wa al-Qaeda, na kuonya kuwa operesheni zao mara nyingine husababisha madhara kwa Waislamu, na kwamba kuungana na al-Qaeda kungewakosesha Waislamu wa Somalia misaada ya kimataifa ambayo walikuwa wanaiihitaji sana kufuatia miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ingawaje ujumbe wa bin Laden wa tarehe 7 Agosti 2010 kwa Ahmed Abdi Godane (Mukhtar Abu al-Zubayr), emir wa al-Shabaab, uliandikwa kwa lugha angalifu sana, maandishi wa ujumbe huo pamoja na ujumbe nyingine zinaonesha wasiwasi kwa upande wa kiongozi marehemu wa al-Qaeda kuwa al-Shabaab walikuwa wanafanya matendo ambayo yangeweza kuwafarakanisha Wasomali na kikundi hicho. Huu ndio uliokuwa msimamo ulioshikiliwa na sehemu kubwa ya Wasomali, wakiwemo “wanajihadi” maarufu kama vile kiongozi wa zamani wa Hizb ul-Islam, Sheikh Hassan Dahir Aweys, aliyewaonya al-Shabaab hapo Machi juu ya hatari ya kuua Waislamu nchini Somalia.

Ushauri wa bin Laden unaonesha kuwa alikuwa anaelewa utumiaji wa adhabu ya hadd uliokuwa unafanywa na al-Shabaab – kuwakata mikono wezi, kuwapiga mijeledi watumiaji wa qat na watu waliokuwa wanaangalia televisheni – kungewafanya wananchi kuwageuka.

Ingawaje bin Laden hakuelezea wazi wazi hali ya maamuzi yake katika ujumbe wake kwa al-Zubayr, alionesha wazi kabisa katika barua kwa kiongozi wa al-Qaeda Atiyah Abdul Rahman hapo mwezi Aprili 2011.

“Ingekuwa vyema kuwapelekea ujumbe ndugu zetu wa Somalia kuhusu faida za kutumia shaka linapokuja suala la kushughulikia uhalifu na utumiaji wa Sharia, sawa na vile alivyosema Mtume, kutumia dhana ili kuacha kuadhibu,” bin Laden aliandika, akikusudia tafsiri ya Sheria ya Kiislamu inayokataza utumiaji mkali wa adhabu ya hadd iwapo kuna shaka yoyote kuhusu mashitaka ambayo yanamkabili mshukiwa.

Ujumbe wa bin Laden kwa kiongozi wa al-Shabaab zinafishua pia kuwa alikuwa na shaka kuhusu operesheni za kikundi cha kijeshi cha Somalia. Mashambulizi ya kikundi hicho mara nyingi hupelekea mauaji miongoni mwa raia wa Somalia ambao hawahusiki na mzozo huo.

“Kuhusiana na mashambulizi yenu kwa Vikosi vya Afrika, lazima muyapitie upya ili kupunguza (madhara) kwa Waislamu kutokana na shambulizi lao zito dhidi ya soko la Bakara,” bin Laden aliandika.

Taratibu za al-Shabaab za kulenga mashambulizi kwa sasa haujabadilika hata baada ya kikundi hicho kulazimishwa kuuhama mji mkuu wa Mogadishu. Kuna taarifa za mara kwa mara za ulipuaji wa mabomu unaofanywa na al-Shabaab ambao unasababisha vifo vingi vya raia, yakiwemo yale ya tarehe 14 Aprili ambayo yalilenga Jumba la Taifa la Maonesho lhuko Mogadishu.

Nyaraka hizo zinaonesha kuwa uamuzi wa bin Laden wa kukataa ombi la al-Shabaab kuwa tawi rasmi la al-Qaeda halikukubaliwa sana ndani ya uongozi wa al-Qaeda. Ujumbe unaoaminika kuandikwa mwezi Disemba 2010 na Ayman al-Zawahiri ulimtaka bin laden kufikiria upya uamuzi wake wa kukataa ombi la al-Shabaab kuwa tawi rasmi la al-Qaeda.

Mnamo mwezi Februari, al-Zawahiri, aliyemrithi bin Laden, na kiongozi wa al-Shabaab al-Zubayr walitangaza kuwa kikundi cha Somalia kilikuwa mshirika rasmi wa al-Qaeda katika Afrika Mashariki.

Haijulikani wazi iwapo kikundi cha al-Shabaab, ambapo sasa shaka za bin Laden juu ya baadhi ya vitendo vyao imefichuliwa, watabadilisha baadhi ya sera zao za msimo mkali. Operesheni zao katika miezi michache hivi karibuni zinaonesha kinyume chake.
Iraki, Pakistan na Yemen

Waraka mwengine uliopatikana katika nyumba ya bin Laden, uliandikwa na Adam Gadahn, mwanachama wa al-Qaeda mwenye asili ya Marekani, ni ujumbe muhimu sana.

Gadahn alitaja mfululizo wa matendo ya matawi ya al-Qaeda na washirika wake na kutaka kuitenganisha al-Qaeda kutoka vikundi hivyo kwa sababu kwa maoni yake vilikuwa vinakiuka mafunzo ya Kiislamu.

Mwandishi wa ujumbe huo anatoa orodha ya mifano ya ulipuaji mabomu ambapo raia wa Pakistani, Afghanistani na Somalia waliuawa. Gadahn alinukuu matukio yaliyomhusisha yeye mwenyewe na kuonesha hamu ya baadhi ya wanajihadi kutaka kupiga mabomu misikiti kwa kisingizio kuwa wasimamizi wake walikuwa si Waislamu wa kweli.

“Inaeleweka kuwa kuishambulia misikiti na kumwaga [damu za] watu wasio na hatia kulikuwa kunajulika katika historia kuwa kulihusishwa na vikundi viovu na watu binafsi,” Gadahn aliandika. “Sasa, wale walio maarufu kwa matendo kama haya hawachukuliwi kuwa ni sehemu ya mujahidina, kama vile Hamas na Talibani wa Pakistani na Afghanistani.”

“Sina shaka kuwa kile kinachotokea katika kikundi cha wanajihadi katika nchi hizi si bahati mbaya bali ni adhabu ya Mungu dhidi yetu kwa sababu ya dhambi na udhalimu wetu, au kwa sababu ya dhambi za baadhi yetu na kimya cha baadhi yetu,” aliongeza.

Haijulikani wazi kuwa ujumbe huu ulikuwa na athari kwa bin Laden kwa sababu katika ujumbe mwengine ambao ulipatikana nyumbani kwake, Atiyya Abdul Rahman na Abu Yahya al-Libi walimuandikia kiongozi wa Talibani wa Pakstani Hakimullah Mehsud, wakishutumu vikali vitendo vya Talibani wa Pakistani kwa madai ya kukiuka mafunzo ya Kiislamu, hasa “kuua Waislamu katika operesheni za kujitoa muhanga yanayotokea katika sehemu za masoko, misikiti, barabarani [na] mikusanyiko ya watu”.

Ukosoaji mkali wa al-Qaeda kwa Talibani wa Pakistani ni muhimu kwa sababu wanachama wengi wa al-Qaeda wanaishi Pakistani chini ya hifadhi ya Mehsud.

Ama kuhusu Iraki, inaonesha kuwa uongozi wa al-Qaeda ulikuwa unaelewa kuwa operesheni za al-Qaeda zilikuwa zinasababisha hamaki za watu nchini humo, kuanzia Abu Musaab al-Zarqawi hadi kwa viongozi wa Taifa la Kiislamu la Iraki.

Taifa la Kiislamu la Iraki “ linajulikana – tupende tusipende – kwa watu kama al-Qaeda nchini Iraki,” Gadahn aliandika.

Alisema vitendo na taarifa za Taifa la Kiislamu la Iraki baada ya kupigwa bomu kwa kanisa mjini Baghdad hapo mwezi Oktoba 2010 hakukukisaidia kikundi hiki kupata huruma za watu badala yale kulipelekea kutengwa zaidi.

“Ni haki ambayo tunazungumza na kile ambacho sheikh [bin Laden] anazungumza katika tarifa na ujumbe zake?” Gahadn aliandika, na kukosoa undumilakuwili baina ya misimamo ilitangazwa na viongozi wa al-Qaeda wanaotetea haki kwa upande mmoja, kwa upande mwingine, vitendo vya matawi ya al-Qaeda wanafanya kinyume sana na matamshi hayo.

Ujumbe hizi ambazo zilikamatwa kutoka nyumbani kwa bin Laden zinajumuisha ukosoaji aliotoa dhidi ya tawi la kikundi hiki nchini Yemeni kwa mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya vikosi vya serikali. Alikubali kuwa matendo kama hayo yanaweza kuyafanya makabila ya Yemen kukigeuka kikundi hiki, jambo lililotokea katika maeneo kadhaa ambako wazee wa makabila waliungana na serikali kukabiliana na mashambulizi ya al-Qaeda.
Kujipa jina jipya

Ni wazi kuwa kutoka na ukosoaji wote huu ambapo bin Laden alikuwa anaelewa kiwango cha madhara kutokana na matendo ya matawi ya jumuiya yake ulimwenguni kote yalikuwa yanasababisha, mabao yaliyoharakisha kufikiria kubadilisha jina, ikiwa ni pamoja na kubadilisha jina la al-Qaeda. Lakini kufanya hivyo kungekuwa na faida gani ikiwa matawi ya jumuiya hayakubadilisha matendo yao?

Bila ya shaka faida ingekuwa ndogo, kwa vile tawi la al-Qaida katika Rasi ya Arabuni sasa inatumia jina la Ansar al-Sharia katika hatua ambazo ni wazi wanatafuta kuungwa mkono na watu. Hata hivyo, kukataa kwa kikundi kuacha kutumia adhabu za hadd na kufanya operesheni zinazoua askari na raia na kuhatarisha kuenea kwa kulaaniwa na umma, kunatoa ushahidi wa wazi kuwa ubadilishaji wa juu juu katika muonekano hakupelekei kwa mabadiliko ya kweli isipokuwa tu kutaambata na mabadiliko ya matendo yao pia.

Views: 406

Tags: Bin, Laden, Nyaraka, al-Qaeda, baina, mvutano, na, wake, washirika, ya, More…za, zafichua

Comment

You need to be a member of G5 world to add comments!

Join G5 world

Comment by raybancheap on May 17, 2012 at 8:42am

A array of Mulberry Shopping bags Mulberry Bags for females contains a different stylish plastic bags great for the fall and even winter seasons. Mulberry is surely an The english language based mostly service which causes a Mulberry UK specialized variety of designer handbags for ladies several of which are restricted style. The product regarding Mulberry Factory Shop Mulberry Hand bags for female drip a way diet and lifestyle which could easily be toted because of simple to Mulberry Handbags help you internet business by using little effort. In fact, the product range involved with Mulberry handbags for women seems to have Mulberry Outlet such type of varied collection there's Mulberry Sale guaranteed to turn into a Mulberry Outlet Store purse for anyone instances.

Comment by Mawazo Katota on May 15, 2012 at 10:44am
Kazi kweli kweli.Haya mambo lazima ya wepo. Sheria yeyote inapotumiwa kinyume na makusudio hugeuka kuwa jinamizi kwa raia ambao wanapaswa kuwa walengwa na wanufaika wa sheria husika. Alqaeda imekuwa ikilaumiwa kila mara yanapotokea mashambuluzj ya maangamizi. Swali ni je hali hii ni ya kwelui na itaendelea hadi lini?

© 2015   Designed & Developed by G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

#ContentAdverts{ width:488px; float:center; margin-right:15px; }